KARIBUNI HABARIMPYA.COM

TOP BANNER1

Tafuta Habari

Thursday, 07 November 2013 07:35

Maisha ya Zitto Kabwe yako hatarini (2)

Written by 
Rate this item
(5 votes)

           Dar es Salaam,Tanzania

KATIKA makala yetu ya tarehe 4 November mwaka 2013 saa 12:47 jioni, toleo namba 3159 Habarimpya.com iliandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari iliyosomeka kwamba 'Njama za kumtimua Zitto Kabwe zinasukwa', katika makala haya nilizungumzia mambo kadha wa kadha kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Moja ya mada kubwa iliyokuwa katika makala hayo ni pamoja na njama zinazopangwa na Chadema kumtimua Zitto kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kufika, Makala hayo yalisomwa na 718 huku watu 60 wakii LIKE pamoja na wengine wengi wakitoa maoni yao katika ukurasa wetu wa Facebook na katika mitandao mingine ya kijamii.

Jana tulikuwa na makala nyingine inayozungumza njama za Chadema kumchafua Zitto Kabwe, baada ya Habarimpya.com kupta ripoti inayozungumzia namna ambavyo maisha ya Mbunge huyo yalivyo wekwa habarini na Chadema, katika makala ya hayo tuliishia hapa, Chombo chetu cha ujasusi tulichokipandikiza kwa siri katika nyendo zote za Zitto Kabwe na ndani ya vikao vya mwanzo kabisa vya Zitto na viongozi serikalini, nahata vile vikao muhimu vya idara ya ujasusi ya chama cha mapinduzi (ccm), kinatupa fursa ya kuweka msingi wa kuimarisha chama cha CHADEMA na kutenda haki kidemokrasia kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla: Endelea kupata dhana halisi kuhusu namna ambavyo ,Maisha ya Zitto Kabwe yalivyo hatarini, ili kusoma sehemu ya kwaza bofya maandishi wa Blue hapo mbele, Maisha ya Zitto Kabwe yako hatarini

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC

Mnamo Jumatatu ya tarehe 16/6/2008 saa 09:46 asubuhi, Mh Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +255754787550 alipokea simu kutoka kwa Ramadhani Ighondu mwenye namba +255717760473 ambaye ni afisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi ikulu hivi sasa. Alijitambulisha kuwa yeye ni Usalama wa Taifa ametumwa na mkuu wake wa kazi aje aongee na Zitto, Maelezo ya msingi katika simu hii ilikuwa ni bwana Ramadhani Ighondu kuomba miadi ya kuonana kutokana na agizo la mkuu wake wa kazi.

"Siku sita baadae yaani Jumatatu ya tarehe 23/6/2008 saa 07:52 asubuhi, Zitto alipigiwa tena simu na Ramadhani Ighondu akimkumbusha maongezi yao waliyo fanya siku 6 zilizopita na kumuomba siku hiyo jioni waonane, ingawa Zitto alionekana kusita kidogo lakini baadae alikubali, Walikubaliana wakutane Sea Cliff Hotel, ilipofika jioni ya siku hiyo Zitto akiwa na marafiki zake wawili Omar Lyasa na Abdalah Said walifika Sea Cliff Hotel wakaketi na kuagiza vinywaji, Baada ya kama dakika kumi hivi Zitto alipokea simu ikimuelekeza alipo bwana Ramadhani Ighondu kisha Zitto akawaambia marafiki zake wamsubiri kidogo, akaondoka kuelekea aliko elekezwa….." ilisema sehemu ya taarifa hiyo, (Kuhusu njama za kutimuliwa kwenye chama bofya maandishi ya bluu), Njama za Mbowe kumtimua Zitto zafichuka

Taarifa hiyo iliyoanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilifafanua kwamba, Mashariki mwa lango kuu la kuingilia Sea Cliff Hotel mita kama tatu tu kuna mlango mdogo unaoelekea kwenye vyumba maalumu (VIP), chumba namba 8 ndicho Zitto alichokuwa anaelekezwa kwa simu kuingia, chumba hiki kina meza moja na sofa zilizo zunguka meza ile zenye uwezo wakukaliwa na watu watano hadi sita, Ndani ya chumba kile Zitto anakutana na watu watatu ambao ni Steven Wasira, Ramadhani Ighondu na Abdalla Punja (hawa wote ni TISS)

Ilisema, Mazungumzo yao ndani ya chumba hiki yalianza maramoja, akianza Mr Ighondu kueleza sababu za wao kumuita Zitto, kikubwa ilikuwa ni “bwana Zitto, serikali (ikulu) inakutaka uache kuibana na kuishurutisha hasa kwa hili suala la Buzwagi”. Tunaomba kujua shida yako kubwa ni nini?” Ighondu alihoji, Katika majibu yake Zitto anajibu, “Mimi napigania haki za watanzania, nimechaguliwa na wanakigoma na watanzania wameniamini ni wawakilishe hivyo”, Lakini mashambulizi ya ushawishi yalipozidi Zitto alilegeza msimamo wake.

Endelea kutembelea habarimpya.com ili kufahamu undani wa mipango ya Chadema kumtimua Zitto Kabwe, jinsi ambavyo maisha yake yalivyo hatarini.

Read 2986 times Last modified on Thursday, 07 November 2013 09:09

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.