KARIBUNI HABARIMPYA.COM

TOP BANNER1

Tafuta Habari

Wednesday, 02 January 2013 15:05

Bongo muvi kumzika Sajuki Dar es Salaam

Written by 
Rate this item
(1 Vote)

Waombolezaji wakimfariji mke wa marehemu Sajuki,Wastara Sajuki aliyejifunika na kanga,nyumbani kwa marehemu Tabata Bima jijini Dar es Salaam.Picha na Jackson Odoyo             Dar es Salaam

WASANII wa filam nchini (Bongo Move) wamefanikiwa kuishawishi familia ya Marehemu Juma Kilowoko maarufu kwa jina la (Sajuki) na kukubaliana na nia yao ya kumzika msanii huyo jijini Dar es Salaam.

Sajuki alifariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu baada ya kuanguka akiwa jukwaani jijini Arusha kwenye ziara ya kuchangisha pesa za matibabu.

Hata hivyo akiendelea na matibabu Hospitalini hapo,jopo la Madaktari walibaini kwamba msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya ngozi,marehemu ameacha mke na mtoto mmoja wa miezi tisa.

Akizungumza Habarimpya.com Rais wa Shirikisho la Filam nchini, (TAFF) Simon Mwakifwamba alisema kwamba, familia ya marehemu imekubaliana na ombi lao la kutaka mwenzao azikwe jijini Dar es Salaam.

“Nikweli kwamba familia ilitaka kwenda kumzika marehemu kijijini kwao Songea, lakini tukawaomba na wakakubalina na ombi letu na tayari tumeshapanga siku ya mazishi kwa kushirikiana na familia,marehemu Sajuki atazikwa katika makaburi ya Kisutu siku ya Ijumaa majira ya saa tano asubuhi”alisema, Mwakifwamba.

Waombolezaji wakimfariji mama mzazi wa marehemu Sajuki aliyelala chini,nyumbani kwa marehemu,Tabata Bima jijini Dar es SalaamHistoria fupi ya Sajuki.

Akizungumza na Habarimpya.com Kaka wa marehemu Salum Kilowoko alisema kwamba, Marehemu alizaliwa April 14 1986 na kuanza elimu ya msingi mwaka 1994 katika shule ya msingi Sokoine na kuhitimu mwaka 2000.

“Marehemu alianza elimu ya Sekondari mwaka 2001 nakuhitimu mwaka 2004 katika shule ya Luhuiko mjini Songera,baada ya hapo aliamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Chuo cha Sanaa cha Kaole mjini Bagamoyo mwaka 2006 na kuhitimu masomo yake mwaka 2007”alisema Salumu Kilowoko.

Alisema kwamba, familia iliamua kumpeleka marehemu katika chuo hicho kwa sababu walibaini kwamba alikuwa na kipaji cha uigizaji tangu akiwa mdogo, lakini kwakuwa alikuwa kijijini kibaji chake akikuweza kufahamika mara moja kwa watanzania.

Marehemu Sajuki enzi za uhai wakeMarehemu Sajuki alianza kujulikana katika tasnia ya filamu nchini mwaka 2008, baada ya kutoa filamu ya Mboni Yangu waliofanya na mkewe Wastara Juma Kilowoko, ikafuatiwa na Two Brothers na Vitamkonaye zote akiwa na mkewe Wastara.

Sajuki alianza sanaa katika kundi la jumba la dhahabu kabla ya kuanza kuandaa filamu zake mwenyewe kupitia Kampuni yake ya Wajey Filamu Production na mpaka mauti yanampata alikuwa na filamu saba huku ya nane ikiwa sokoni na itaanza kuonekana wiki ijayo.

Tovuti ya jamii ya Habarimpya.com itaendelea kuwaletea taarifa mbali mbali na mambo yanayoendelea kujiri katika msiba huo, habarimpya.com pia inaendelea kuwaletea makala ya mwenendo wa kesi ya msanii wa fialmu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) anaye kabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba bila ya kukusudia, kamala haya yanawajia kila siku ya Jumatatu,Jumatano na Ijumaa.

Habarimpya.com pia inaendelea kuwaletea mwendelezo wa makala za Falsafa za Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zinazorushwa hewani kila siku ya Jumapili.

Read 1131 times Last modified on Wednesday, 02 January 2013 18:46

Leave a comment

Make sure you enter the (*) required information where indicated. HTML code is not allowed.